Taarifa ya Hizbullah imevitaja vikwazo hivyo vya madola ya kibeberu dhidi ya Iran na Siria kuwa ni vya kichochezi na visivyokuwa vya kiuadilifu. Taarifa hiyo ya Harakati ya utetezi wa Kiislamu ya Lebanon imeongeza kuwa, vikwazo hivyo dhidi ya Iran na Siria ni katika njama nyingine za Wamagharibi za kutaka kuchochea chuki dhidi ya nchi za Kiislamu za Mashariki ya Kati. Hizbullah imeutaka ulimwengu wa Kiislamu kuwa macho na njama hizo ili kudumisha umoja na mshikamano wake. Novemba 21, Marekani, Uingereza na Kanada zilipasisha vikwazo vipya dhidi ya sekta ya nishati na Benki Kuu ya Iran kutokana na ripoti iliyotolewa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA mnamo Novemba 8, iliyokariri tuhuma zisizo na msingi kuwa miradi ya nyuklia ya Iran imepoteza mkondo na kuwa inaelekea kuwa na malengo ya kijeshi.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 281963
Harakati ya utetezi wa Kiislamu ya Lebanon Hizbullah imekosoa hatua ya Wamagharibi ya kuiwekea vikwazo vipya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.